Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Hawza kutoka Tehran, ujumbe wa Mtukugu Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwa mnasaba wa siku arubaini tangia kuuawa kishahidi Kiongozi Mkuu mtukufu wa Mapinduzi (ra) na masuala muhimu yanayohusiana na vita ya tatu ya kulazimishwa, umechapishwa.
Matini kamili ya ujumbe huu ni kama ifuatavyo:
بسم الله الرحمن الرحیم
إِنَّا فَتَحْنَا لَکَ فَتُحَامُبِینَا لِیَغْفِرَ لَکَ الله ما تَقْدَّمَ مِن ذنبکَ وَمَا تَأَخَرَ وَیُتِمْ نِعْمَتَهُ عَلَیْکَ وَیَهْدِیکَ صِراط مستقیماً وینصرکَ اللَّهُ نَصْراً عَزیزاً.
Zimepita siku arubaini tangu kutokea moja ya jinai kubwa kabisa zilizofanywa na maadui wa Uislamu nchini Iran, na mojawapo ya majonzi mazito zaidi ya umma katika historia ya taifa hili, ni msiba wa kuuawa kishahidi kwa uchungu mkubwa wa Kiongozi Mkuu mtukufu wa Mapinduzi ya Kiislamu, baba wa taifa la Iran, kiongozi wa Umma wa Kiislamu, na muongozi wa wanaotafuta haki katika zama hizi, Sayyid wa mashahidi wa Iran na wa Jamhuri ya Muqawama, Khamenei Mkuu (ra)
Zimepita siku arubaini tangu roho tukufu ya kiongozi wetu shahidi iwe ngeni katika ukaribu wa Mwenyezi Mungu, katika karamu ya mawalii, wasadiki na mashahidi; na wakati huo huo au baada yake, idadi kubwa ya marafiki, makamanda na wapiganaji wa Uislamu, pamoja na wananchi wanyonge wa nchi hii — kuanzia watoto wachanga hadi wazee — nao wamefikia neema hii kubwa.
Kwa siku arobaini mchana na usiku, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemwita kiongozi wa umma huu kwenye miadi yake; lakini safari hii, tofauti na yaliyotokea, wafuasi wa kiongozi shahidi na umma wake wametumwa kwa ajili ya kusimamisha haki na kupambana na batili, na wamesimama imara kama milima dhidi ya Samiri na ndama wake, na kama lava ya moto wamewashukia wavamizi na Mafirauni.
Kwa siku arubaini mchana na usiku, madhalimu wakubwa wa dunia wameondoa nyuso zao za hadaa na za uongo, na kuonesha sura zao chafu na za kishetani za mauaji, dhulma, uvamizi, uongo, kiburi, kuua watoto, udikteta na ufisadi.
Lakini kwa upande mwingine, kwa siku arubaini mchana na usiku, watoto mashujaa wa Khomeini Mkuu na Khamenei mpendwa shahidi, na wafuasi wa Uislamu halisi wa Muhammad (saww), wamehudhuria kwa juhudi na ushujaa wa mfano katika viwanja, mitaa na ngome za mapambano, na licha ya madhara na hasara za mashambulizi ya kinyama ya adui, wameibadilisha vita ya tatu ya kulazimishwa kuwa uwanja wa mashujaa wa utetezi mtakatifu wa tatu. Taifa la Iran lenye uelewa na tahadhari, ingawa limeonesha kuwa lina huzuni kubwa kwa kumpoteza kiongozi wake shahidi, lakini kwa kufuata warithi wa moja kwa moja wa Ashura ya Husseini, limegeuza huzuni hii kuwa ushujaa, na maombolezo kuwa kauli za kishujaa; na yote haya yamewaacha maadui wenye silaha katika mshangao na kukata tamaa, na yamewalazimisha watu huru duniani kuwapongeza. Safari hii ujinga wa madhalimu ulisababisha kwamba Esfand 1404 (Mwezi wa Shamsiya) uwe mwanzo wa zama mpya wa kuinuka kwa jina la Iran na Mapinduzi ya Kiislamu, na bendera ya Iran ya Kiislamu ipandishwe si tu katika jiografia ya nchi yetu bali pia katika vilindi vya nyoyo za wanaotafuta haki duniani.
Sifa na sanaa za Kiongozi Shahidi
Mnasaba huu ni fursa nzuri ya kumtambulisha kwa ufupi kiongozi huyu mtukufu. Tunamzungumzia mtu ambaye, licha ya umaarufu wake, hakutambulika ipasavyo. Wote wanajua kuwa kiongozi wetu shahidi alikuwa faqihi mwenye kutambua zama, mwenye basira, mpiganaji asiyechoka, imara kama mlima, mwanachuoni mwenye kutenda na wa kiroho, mtu wa dhikr, tahajjud, unyenyekevu mbele ya Mola, na mwenye kutawassal kwa Maimamu watakatifu (as), na kwa kina cha moyo wake alikuwa na imani na ahadi za Mwenyezi Mungu.
Miongoni mwa sifa zake nyingine ilikuwa mapenzi kwa Iran na juhudi endelevu za kuifanya iwe huru zaidi, pamoja na kusisitiza umoja na mshikamano wa kitaifa. Alitumia maisha yake yote katika kuanzisha, kuimarisha na kudumisha mfumo wa Kiislamu, na kwa mtazamo wake, Jamhuri ya Kiislamu bila watu haikuwa na maana.
Pamoja na uimara na nguvu, alikuwa na umakinifu mkubwa katika fikra na mtazamo. Aliangalia kwa makini uwezo wa nchi hasa vijana. Alitoa umuhimu kwa elimu, teknolojia na maendeleo. Alithamini sana familia za mashahidi, majeruhi na wapiganaji waliojitoa muhanga. Alikuwa na tajriba nyingi zenye thamani katika nyanja mbalimbali, baadhi yake zikiwa na historia ya miongo kadhaa, pamoja na sifa nyingine nyingi.
Katika siku hizi, vyombo vya habari mara kwa mara vinazungumzia kuhusu sanaa na ufahamu wake wa sanaa. Ingawa kipengele hiki pekee kinaweza kumpa mtu thamani kubwa, na bila shaka kilikuwepo kwa kiwango cha juu kwake, lakini kikilinganishwa na sifa zake nyingine kinaonekana kidogo. Mimi binafsi najua sanaa nyingi alizokuwa nazo; mojawapo ya sanaa zake kubwa ambayo haijazingatiwa sana ni uwezo wake wa kulea na kuiunda jamii kupitia ujenzi wa fikra, hisia na nafsi za umati mkubwa wa watu na makundi ya kijamii.
Sanaa nyingine ilikuwa uundaji wa taasisi kwa malengo maalum, hasa katika miaka ya mwanzo ya uongozi wake, akiwa na mtazamo wa mbali.
Sanaa nyingine ilikuwa kuimarisha nguvu ya miundo ya kijeshi ya nchi, ambayo taifa la Iran limefaidika nayo katika vita mbili za kulazimishwa za karibuni. Pia alikuwa na uwezo wa ubunifu katika nyanja za kielimu, kimkakati na kisera, kama inavyoonekana katika sera kuu za mfumo. Aidha alikuwa na uwezo wa kuumba maana kupitia maneno mapya na mchanganyiko wa kipekee wa maneno, ambayo yalizalisha na kubeba maana nyingi, na kuunda mjadala wa kijamii.
Na miongoni mwa sanaa zilizotokana na kusafishwa kwa roho yake katika mitihani na taabu, kutokana na subira na ustahimilivu katika njia ya haki, ilikuwa ni uwezo wa kutabiri matukio ya mbali:
«المؤمن ینظر بنور الله»
Na sanaa nyingine nyingi ambazo haiwezekani kuzihesabu hapa kwa ufupi.
Sifa hizi zote zilikuwa na chanzo katika neema maalum za Mwenyezi Mungu na uangalizi wa mababu zake watakatifu (sa). Inawezekana sababu ya neema hizi ilikuwa juhudi zake za dhati na zisizokoma katika kuliinua neno la haki.
Hata hivyo, kwa namna ya pekee, mbali na magumu ya mapambano dhidi ya mfumo wa khaini wa utawala wa Pahlavi, yeye pia alifaidika sana na fursa nyingine maalum katika njia ya kutekeleza wajibu wake, ambayo kwa kawaida watu wengi hawajui. Ilikadiriwa hivi kwamba kijana huyo Sayyid aliyekuwa na shauku kubwa ya elimu na pia mwenye kutaka kutenda, wakati baba yake mtukufu alipokuwa katika hatari ya kupoteza uwezo wa kuona, baada ya miaka mingi ya kupiga magoti mbele ya walimu wakubwa, aliacha mazingira yote ya nje ya maendeleo ya kielimu na mustakabali wake huko Qom, na kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, akajitoa kikamilifu kumhudumia baba yake.
Neema ya Mwenyezi Mungu ilidhihirika baada ya kujitolea huku kwa namna hii kwamba ghafla Sayyid Ali Khamenei katika umri wa chini ya miaka thelathini aliibuka kama jua kutoka Khorasan, na kwa haraka akawa mmoja wa nguzo za fikra na mapambano, na wakati huo huo akapata maendeleo makubwa katika elimu za kawaida; kiasi kwamba katika miaka ya hamsini, taasisi ya SAVAK ilimwita “Khomeini wa Khorasan”. Ni lazima kusisitiza kwamba mchakato huu wa maendeleo ya ndani na ya nje wa mtu huyu mtukufu uliendelea pia katika hatua zilizofuata.
Sasa katika kujifunza kutokana na mwenendo wa wakubwa, hasa mtu wa aina hii, ni jambo linalofaa sana kufanya sifa ya kuwahurumia wengine kwa dhati na kusaidiana kuwa ndio mwenendo wetu. Sifa hii, pamoja na kuzingatia rehema pana ya Mwenyezi Mungu, ndiyo tofauti kuu kati ya anayesimama chini ya bendera ya haki na wale wanaokusanyika chini ya bendera ya batili. Bila shaka, kufuata mwenendo huu kutafungua milango ya mbinguni na kushusha aina mbalimbali za msaada wa Mwenyezi Mungu na wa ghaibu; kuanzia kunyesha kwa mvua ya rehema hadi kushinda adui na hata maendeleo ya kielimu na kiteknolojia.
Katika siku hizi mara kwa mara inasikika kwamba makundi mbalimbali ya watu wapendwa, kwa haki na kwa huzuni, wanakumbuka zama zile za kipekee, na polepole sura nyingi zaidi za lulu ya kung’aa ya haiba yake tukufu zinaonekana. Pia azma ya kufuata baadhi ya matendo yake inazidi kuwa ya kawaida; miongoni mwa hayo, watu wetu wapendwa wamejifunza kutokana na ngumi iliyokunjwa ya kiongozi huyo wakati wa kuuawa kwake kishahidi, na sasa ngumi hiyo imekuwa kwa baadhi kama alama ya pamoja ya itikadi.
Hivi ndivyo inavyothibitika tena kwamba; athari ya shahidi ni kubwa zaidi kuliko mtu aliye hai, na sauti yake yenye nguvu katika wito wa tauhidi, kutafuta haki na kupambana na dhulma na uharibifu ni yenye mwangwi mkubwa zaidi, na ujumbe wake una athari kubwa zaidi kuliko wakati wa uhai wake. Aidha, matamanio ya moyoni ya shahidi huyu mtukufu kuhusu ustawi wa taifa hili na mataifa mengine ya Kiislamu sasa yako karibu zaidi na kutimia kuliko hapo kabla.
Ushindi wa taifa shujaa la Iran katika vita ya tatu ya kulazimishwa
Ndugu zangu wa kiume na wa kike, wananchi wenzangu; hadi hatua hii ya tukio la utetezi mtakatifu wa tatu, kwa ujasiri kabisa inaweza kusemwa kwamba; nyinyi taifa shujaa la Iran, ndio washindi wa hakika katika uwanja huu.
Leo mwanzo wa kuinuka kwa Jamhuri ya Kiislamu kama nguvu kubwa na kuingia kwa madhalimu katika mteremko wa udhaifu umeonekana wazi mbele ya macho ya wote. Bila shaka hii ni neema ya Mwenyezi Mungu iliyotokana na baraka ya damu ya kiongozi wetu shahidi na mashahidi wengine waliovaa sanda nyekundu ya damu, na wananchi wanyonge, na watoto waliouawa wa shule ya Shajarat Tayyiba ya Minab, pamoja na dua na unyenyekevu wa wananchi wote mbele ya Mola, na uwepo wao wa kishujaa katika viwanja, mitaa na misikiti, na kwa sababu ya kujitolea kwa dhati kwa wapiganaji wa Uislamu katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi, jeshi la nchi, vikosi vya usalama, askari wasiojulikana na walinzi wa mipaka.
Neema hii pia, kama neema nyingine yoyote, inapaswa kushukuriwa ili iendelee na kukua:
«لَئِن شَکَرتُم لَأَزِیدَنَّکُم»
Shukrani ya kivitendo kwa neema hii ni juhudi zisizokoma za kuifikia Iran yenye nguvu.
Umuhimu wa kuendelea kwa uwepo wa wananchi
Jambo muhimu katika hatua ya sasa kwa ajili ya kufikia lengo hili la kimkakati la kiongozi shahidi ni kuendelea kwa uwepo wa wananchi kama ilivyokuwa katika siku arobaini zilizopita. Uwepo huu ni nguzo muhimu ya hadhi ambayo Iran yenye nguvu imeifikia.
Hivyo basi, haitakiwi kufikiri kwamba; kwa kutangazwa kwa uwezekano wa mazungumzo na adui, uwepo wa watu mitaani hauhitajiki. Bali hata kama kwa dharura hatua ya kimya katika uwanja wa vita imefika, wajibu wa wananchi ambao wanaweza kuhudhuria katika viwanja, mitaa na misikiti ni mkubwa zaidi kuliko hapo kabla.
Bila shaka sauti zenu katika viwanja ina athari katika matokeo ya mazungumzo; kama ilivyo pia kwa idadi kubwa inayoongezeka ya kampeni ya “Kujitolea kwa ajili ya Iran”, ambayo ni miongoni mwa mambo yenye athari katika uwanja huu. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kwa kuendelea kwa mchango huu, mustakabali unaongojea taifa la Iran ni zama za utukufu, mwanga, heshima na ustawi.
Mambo kuhusu majirani wa kusini, fidia na damu ya mashahidi
Katika nafasi hii, ninawaambia majirani wa kusini wa Iran: mnashuhudia muujiza. Basi muone vizuri, eleweni vizuri, na msimame mahali sahihi, na muwe na tahadhari dhidi ya ahadi za uongo za mashetani. Bado tunangoja majibu yanayofaa kutoka kwenu ili tuwaoneshe undugu na nia njema.
Hili haliwezi kutokea isipokuwa kwa kujitenga kwenu na madhalimu ambao hawakosi fursa ya kuwadharau na kuwanyonya. Wote wanapaswa kujua kwamba; kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hatutawaacha wavamizi walioitendea nchi yetu uhalifu. Hakika tutadai fidia ya kila hasara iliyosababishwa, na damu ya mashahidi, na malipo ya majeruhi wa vita hii. Pia bila shaka tutaupeleka usimamizi wa Mlango wa Hormuz katika hatua mpya.
Sisi hatukutaka vita wala hatutaki, lakini kamwe hatutaacha haki zetu halali, na katika hili tunaiangalia kwa umoja Jamhuri ya Muqawama.
Mapendekezo kwa wananchi wote
Katika kipindi hiki hadi kufikia haki zetu:
Kwanza, wananchi wote wajitahidi kuzingatia hali ya wenzao ili kupunguza shinikizo linalotokana na upungufu wa kawaida wa vita. Hata hivyo, upungufu huu, ambao kwa upande wa adui ni mkubwa zaidi, kwa juhudi za serikali na taasisi nyingine umeweza kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa.
Pili, kulinda masikio yetu — ambayo ni dirisha la akili na moyo — dhidi ya vyombo vya habari vinavyoungwa mkono na adui au vinavyokwenda sambamba naye ni jambo la lazima. Bila shaka vyombo hivyo si vyenye nia njema kwa taifa la Iran. Hivyo ima tuepuke kabisa, au angalau tuvitazame kwa tahadhari kubwa.
Tatu, taifa hili tukufu, ingawa baada ya kumalizika kwa kipindi rasmi cha maombolezo litaacha mavazi ya huzuni, lakini litadumisha azma thabiti ya kulipiza kisasi damu ya kiongozi wake shahidi na mashahidi wote wa vita hii.
Mwisho, ninamwelekea bwana wetu (ajtf) nikisema: sisi kwa kumuamini Mwenyezi Mungu na kwa kutawassal kwa Maimamu (as)، na kwa kumfuata kiongozi wetu shahidi, tumesimama chini ya bendera yenu dhidi ya kambi ya ukafiri na ubeberu. Katika njia hii tumetoa mashahidi wengi kutoka tabaka mbalimbali na tumepata hasara pia.
Sasa kwa moyo wote tunategemea dua maalum yenu kwa ajili ya ushindi kamili dhidi ya adui, iwe katika uwanja wa mazungumzo au katika vita, na tunatumaini kwamba; hivi karibuni sisi na maadui wetu tutaona athari yake ya kimiujiza, inshaallah.
والسلام علیکم ورحمة الله وبرکاته
Sayyid Mujtaba Khamenei
20 Farvardin 1405/ 9 April 2026
Maoni yako